Sports

  Mshambulizi wa timu ya taifa ya Harambee Stars na klabu ya Girona, Michael Olunga ameandikisha historia hii leo baada ya kuwa Mkenya wa kwanza kufunga bao kwenye ligi ya Uhispania Laliga. Aidha, Olunga almaarufu “Engineer ” amekuwa mchezaji wa kwanza wa klabu hiyo ya Girona kufunga mabao matatu kwenye mechi moja. Itakumbukwa kuwa Olunga alijiunga na Girona […]

  Miamba wa Laliga Uhispania, Barcelona wamefanikiwa kumpata Philippe Coutinho kutoka Liverpool kwa rekodi ya Euro milioni mia moja sitini (€100M). Barca wamempata nyota huyo baada ya muda mrefu wa kutuma maombi yaliyokataliwa. Kipindi kilichopita cha uhamisho, kilishuhudia uhamisho wa Coutinho ukigonga mwamba dakika za lala salama, baada ya Liverpool kusema nyota huyo hakuwa wa […]

The team that will represent North Eastern in the Chapa Dimba Na Safaricom national final will be decided this weekend. Garissa University will host the fourth regional final of the youth tournament which aims at scouting for talent, developing grassroots football, and ultimately propelling gifted players to the national team. Four boys teams will take […]

  Mshambulizi wa taifa la Misri na Klabu ya Liverpool , Mohammed Salah ameshinda tuzo la mchezaji bora Afrika, wiki chache baada ya kutwaa tuzo la BBC. Salah ambaye amefunga mabao kumi na saba kwa mechi kumi na tisa za ligi, na matano katika mechi sita za kombe la Klabu Bingwa. Mjukuu huyo wa Firauni aliwapiku […]

  Mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria, Asisat Oshoala alishinda taji la tatu kuwa mchezaji bora Afrika kwa kina dada, usiku wa Alhamisi. Oshoala alitwaa tuzo hilo mwaka wa 2014 na 2016, na hapo jana aliwapiku Gabrielle Aboudi Onguene wa Cameroon na Chrestina Kgatlana wa Afrika Kusini, katika hafla iliyoandaliwa kule Accra, Ghana. Oshola […]

    Wiki jana, jaji wa mahakama kuu ( High Court) Jaji John Mativo alifanya uamuzi si mchache ambapo kampuni ya uwekezaji nchini Sportpesa, ilipoteza kesi ya kupinga ada wanayotozwa na serikali. Sportpesa ilikuwa imelalamikia ada hiyo ya asilimia thelathini na tano (35%) ambayo wanadai ipo juu mno. Kampuni hiyo sasa imetangaza kuondoa ufadhili wake kutoka […]

  Mshambulizi wa Kariobangi Sharks na timu ya taifa Harambee Stars, Masoud Juma amejiunga na klabu ya Afrika Kusini Cape Town City. Klabu hiyo ilitangaza usajili huo katika mtandao wao wa Twitter mapema leo. Hata hivyo hela za usajili hazijawekwa wazi.   Juma amekuwa nguzo muhimu kwa kikosi cha Harambee Stars kilichotwaa taji la CECAFA […]

  Mlinzi wa Southampton Virgil Van Djik atajiunga na Liverpool mwezi Januari tarehe moja kwa rekodi ya paundi milioni sabini na tano (£75M). Nyota huyo wa Uholanzi alifaa kujiunga na The Reds mwezi Julai, ila uhamisho huo ukafeli baada ya kujulikana kuwa Liverpool haikufuata sheria katika kutaka kumsajili. Usajili huo wa Van Djik utakuwa ghali […]

  Mshambulizi wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Tottenham Harry Kane, amevunja rekodi ya mabao thelathini na sita iliyowekwa na Alan Shearer miaka ishirini na mbili iliyopita. Shearer alifunga mabao hayo akiwa na klabu ya Blackburn Rovers mwaka wa 1995. Kane alifunga mabao matatu siku ya Jumanne Tottenham ilipoicharaza Southampton mabao matano […]

  Aliyekuwa kiungo mtengenezaji wa Arsenal na Borussia Dortmund, Tomas Rosicky amestaafu. Gwiji huyo aliyependwa sana kwa mchezo wake wa gusa niguse alitangaza kustaafu hiyo jana, katika maongezi na vyombo vya habari kule Jamhuri ya Czech. Rosicky alisema kuwa ameafikia uamuzi huo kwa kuwa umri wake wa miaka 37 haumruhusu kuendelea kucheza kabumbu ya kulipwa. […]


Campus Radio

Campus Radio

Current track
TITLE
ARTIST

Background