Kwa kweli, ukweli wa kauli hii ulidhihirika usiku wa Jumanne na Jumatano wiki hii kwenye dimba la Kombe la Mabingwa baada ya Borussia Dortmund na Atletico Madrid kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye kipute hicho.

Miamba hao wa Bundesliga, wanasheheni mastaa tajika kama Marco Reus, Pierre-Emerick Aubameyang na Shinji Kagawa ila waliambulia sare tasa ugenini dhidi ya Apoel Nicosia kule Cyprus. Apoel walipata uongozi dakika ya sitini na mbili kupitia kwa Potè kabla ya Sokratis Papastathopoulos kusawazishia Dortmund dakika tano baadaye.
Wajerumani hao walianza kampeni zao vibaya kwenye michuano hiyo kwa kucharazwa na Real Madrid mwezi Septemba kabla ya kurindimwa mabao matatu kwa moja na Tottenham kule Wembley. Dortmund wanaoongoza jedwali la Bundesliga, watakuwa na kibarua nyumbani dhidi ya Apoel na Tottenham mwezi ujao, kabla ya kuchuana na Real Madrid kule Santiago Bernabeu.
Mibabe hao wa Ujerumani, wanavuta mkia kwenye kundi hilo kwa alama moja baada ya mechi tatu na sharti washinde mechi zote za marudiano ili kujikatia tikiti ya kufuzu.

Hali kadhalika, vijana wa Diego Simeone walijitia kikaangoni usiku wa Jumatano baada ya kuambulia sare tasa dhidi ya Qarabag, timu iliyokamilisha mechi watu kumi kiwanjani. Wahispania hao sasa, wamejipata kwenye nafasi ya tatu katika kundi lao kwa pointi mbili baada ya mechi tatu. Hii ni baada ya kutoka sare walipochuana na Roma huku wakipoteza kwa Chelsea mwezi uliopita nyumbani Wanda Metropolitano.
Huku mechi tatu zikiwa zimesalia kwenye awamu ya makundi, kikosi hicho cha Simeone sharti kishinde mechi zote ili kufuzu kwa awamu ijayo. Hilo litawaepusha kutokana na kupiga hesabu ya vidole wakizingatia matokeo ya timu za hayo makundi mengine.
Chelsea wanaongoza kundi hilo kwa alama saba wakifuatwa kwa karibu na Roma walio na pointi tano. Iwapo Atletico watashinda mechi hizo tatu, watafuzu kirahisi kwa alama kumi na moja. Aidha, wakishinda mbili na kupoteza moja na Chelsea ipige Roma, watafuzu kwa msingi wa mabao. Hata hivyo, ikiwa Atletico watashinda mechi mbili na kupoteza moja nayo Chelsea itoke sare na Roma, Wahispania hao watalazimika kuaga michuano hiyo na kucheza ligi ya Europa.
Mshambulizi wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann alikiri kutoridhika na sare hiyo dhidi ya Qarabag huku akiwasihi washambulizi wenzake kumakinika.
“Kama washambulizi sharti tufanye kazi yetu. Tuna walinzi hodari na viungo wanaotengeneza nafasi nyingi. Ni sisi tunaofaa kufunga mabao,” alisema Griezmann.

Yassina Terry.

Wachezaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann (kulia) na Filipe Luis ( kushoto) baada ya sare yao dhidi ya Qarabag.

Leave a Comment