Awamu ya kwanza ya michuano ya KUSA RIFT CONFERENCE ilikamilika hapo jana Oktoba mosi huku vyuo kadhaa vikidhihirisha weledi wao katika mchezo wa soka.Timu ziligawanywa katika vikundi viwili kundi A likichezea Annex kundi B likisakatia UoE.

Kwenye timu za kiume, kundi A lilisheheni timu za Maasai Mara, Egerton Njoro, Kabarak na K.U. Kundi B lilihusisha timu za UoE, Egerton NTC na Laikipia. Kwa kina Dada, kundi A lilisheheni  Egerton Njoro, Moi Main Campus na K.U.huku kundi B likihusisha UoE,Moi West Campus na Laikipia.

Mechi za kwanza zilisakatwa Jumamosi ambapo timu ya Egerton Njoro iliicharaza Kabarak Bao moja kwa nunge bao lililofungwa na Barasa Koyo.Maasai Mara iliinyanyasa KU mabao matano kwa nunge Betto Hassan akifunga matatu, Okuka Ishaque na Kiplagat Collins wakifunga moja moja.Kule UoE, Egerton NTC ilipoteza kwa UoE kwa kichapo cha mabao matatu kwa mawili huku Laikipia ikiambulia sare na UoE. Timu za Egerton Njoro kutoka kundi A zilifuzu kwa nusu fainali huku UoE na Laikipia zikifuzu kutoka kundi B.

Kwa upande wa kina dada, Egerton Njoro iliicharaza Moi Main Campus mabao mawili kwa nunge kabla ya kuinyeshea KU idadi hiyo hiyo ya mabao. Victory Oudu, Roseline Multi, Jackline Musangi na Beatrice Achieng waliifungia Egerton. Timu ya Moi Main Campus ilijikwamua kwa kuilaza KU mawili kwa nunge Daisy na Nancy wakicheka na wavu. UoE nayo iliikanyaga West Campus bao moja komboa ufe huku West Campus wakishindwa kujikwamua dhidi ya Laikipia baada ya kunyukwa bao moja.

Yassina Terry,  

Leave a Comment