Droo ya Kombe la klabu bingwa iliandaliwa leo alasiri huku kipute babu kubwa kikisubiriwa kati ya Real Madrid ya Uhispania na Paris Saint Germain ya Ufaransa.
Chelsea ya Uingereza inakabiliwa na mtihani mgumu dhidi ya Barcelona ya Uhispania huku Tottenham ikitifua kivumbi dhidi ya Juventus.
Timu ya Manchester United itagaragaza dhidi ya Sevilla huku Manchester City ikiwa na kazi nyepesi dhidi ya Basel. Katika hali iyo hiyo, Klabu ya Liverpool chini ya kocha Jurgen Klopp itatifua kivumbi dhidi ya FC Porto kutoka Ureno.
Ligi ya Europa haikusazwa kwani droo ya awamu ya thelathini na mbili ilifanyika pia. Klabu za Dortmund, RB Leipzig,Atletico Madrid na Napoli zilizobanduliwa kutoka Ligi ya mabingwa ziliratibiwa vilevile.
Mchuano mkali utakuwa baina ya Napoli na RB Leipzig, Dortmund ichuane na Atalanta, Atletico nayo igaragaze FC Copenhagen. Arsenal ya Uingereza itachuana na Ostersunds FK katika mtihani unaoonekana mwepesi.