INIESTA KUCHEZEA BARCELONA HADI KIFO
Kiungo wa timu ya taifa ya Uhispania na nahodha wa Barcelona, Andres Iniesta ameikabidhi klabu hiyo maisha yake. Nyota huyo ametia sahihi kandarasi hiyo ya maisha leo, Ijumaa mchana mbele ya raisi wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu.
Iniesta, alijiunga na Barcelona mwaka wa elfu moja kenda mia tisini na sita (1996) akiwa na umri wa miaka kumi na miwili.Kiungo huyo amechezea miamba hao wa Laliga mechi mia sita thelathini na tisa na kufunga mabao hamsini na tano.
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka thelathini na tatu aliibukia kwenye akademia ya Barcelona almarufu La Masia na kuteuliwa kuwa nahodha mwaka wa elfu mbili kumi na tano Iniesta anajivunia mataji thelathini akiwa na Barcelona rekodi sawia na ya Lionel Messi.
Wengi wanamkumbuka Iniesta kwa bao lake la muda wa mazidadi aliloifungia Uhispania dhidi ya Uholanzi na kusaidia timu hiyo kutwaa Kombe la Dunia mwaka wa elfu mbili na kumi kule Afrika Kusini.
-Yassina Terry