Aliyekuwa mlinzi wa Arsenal, Lauren Bisan anatarajiwa kutua anga za Kenya mwezi Desemba mwaka huu kulingana na mtandao wa Goal.. Bisan ambaye ni mzaliwa wa Ivory Coast anakumbukwa kwa kuiongoza nchi yake kutwaa medali ya dhahabu kwenye michuano ya Olimpiki.Lauren pia alikuwa kwenye kikosi cha Arsenal kilichoshinda taji la ligi kuu Uingereza bila kupoteza mechi yoyote.
Nyota huyo mstaafu, atajiunga na makocha wa Arsenal; Drew Taylor, Johnny Georgiou na James Colines waliopo nchini tayari. Lauren atajiunga na watatu hao katika kuendeleza mafunzo ya ukocha ili kuinua hadhi ya Soka nchini.
Kocha wa kikosi cha vijana wasiozidi umri wa miaka ishirini wa AFC Leopards, Boniface Ambani amesema kuwa zoezi hilo litawasaidia mno. Zoezi hilo ambalo limefadhiliwa na kampuni ya uwekezaji ya Sportpesa litang’oa nanga muda wowote kutoka mwezi huu wa Oktoba.
Itakumbukwa kuwa Lauren alikuwa kiungo wa kati kabla ya mkufunzi wa Arsenal, Arsene Wenger kumgeuza kuwa beki wa kati.
Yassina Terry.