“PAMZO” Anyakua Kago na Misiko

Luis Misiko zamani Tusker

 

Klabu ya Posta Rangers inayoshiriki ligi Ku nchini imevamia mabingwa wa 2016 Tusker, na kusajili kiungo wa kati Luis Misiko.

Misiko ametia sahihi mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ambayo ilimaliza ya nne, msimu uliopita. Misiko atajumuika na aliyekuwa mchezaji-mwenza kule Tusker, Danson Kago.

Fauka ya hayo, Rangers wamesajili Jeremiah Wanjala kutoka Kakamega Homeboyz.

 

Kago alijiunga na Rangers mapema wiki jana huku akiandikisha kandarasi ya miaka mitatu vile vile.  Nyota huyo alitemwa na Tusker pamoja na wenzake kumi na tatu wanaojumuisha Alan Wanga.

Hata hivyo, Kago amerejea ulingoni kuchezea klabu yake ya utotoni aliyoiga 2012, na kujiunga na Sofapaka. Baada ya misimu mitatu ya ufanisi na “Batoto ba Mungu, Kago alisajiliwa na Tusker kabla ya kutemwa mwishoni mwa msimu jana.

Kocha wa Rangers, Sammy Omollo “Pamzo”

Kocha wa Rangers, Sammy Omollo “Pamzo” ameonyesha juhudi zake za kushinda taji msimu ujao, kwani amesajili washambulizi wa AFC Leopards; Marcellus Ingotsi, Suleiman Ngotho na Calvin Odongo.

Leave a Comment