Mshambulizi wa taifa la Misri na Klabu ya Liverpool , Mohammed Salah ameshinda tuzo la mchezaji bora Afrika, wiki chache baada ya kutwaa tuzo la BBC.

Salah ambaye amefunga mabao kumi na saba kwa mechi kumi na tisa za ligi, na matano katika mechi sita za kombe la Klabu Bingwa.

Mjukuu huyo wa Firauni aliwapiku mchezaji mwenza wa Liverpool, Sadio Mane na Pierre Emerick Aubameyang wa Gabon, walioibuka wa pili na tatu mtawalia.

Mane, Salah na Aubameyang katika hafla hiyo

 

Salah sasa anajiunga na orodha ya mibabe wa Afrika; Yaya Toure, Didier Drogba na Samuel Eto’o walioshinda taji hilo hapo awali.

Itakumbukwa kuwa Salah aliisaidia Misri kufuzu kwenye Kombe la Dunia, huku akifunga mabao mawili kwenye mechi muhimu dhidi ya Congo.

 

Mane na Salah

Liverpool itachuana na Everton katika kipute kikali cha kombe la FA usiku wa Ijumaa, na licha ya kibarua hicho kocha Jurgen Klopp aliwaruhusu Mane na Salah kuhudhuria hafla ya tuzo hizo.

Hata hivyo, Mane alihitajika kurejea baada ya tuzo hizo huku klabu hiyo ikituma ndege maalum kumrejesha nyota huyo. Hata hivyo, Salah atakosa mechi hiyo kwa kuwa ana jeraha.

 

Leave a Comment