ROYAL ANTWERP YAMPOTEZA CHIPUKIZI; MIAKA 17

Joel Lobanzo

Kifo cha chipukizi wa Ubelgiji Joel Lobanzo, kimeibua majonzi kwenye ulimwengu wa kabumbu, baada ya mchezaji huyo kufariki mazoezini. Lobanzo anayechezea Royal Antwerp aliaga dunia baada ya kupata mshtuko wa moyo katika mazoezi ya kikosi cha vijana wasiozidi miaka kumi na tisa.

Kinda huyo alizimia mwanzo ambapo madaktari wa klabu walimtibu usiku wa Jumanne wiki hii kabla ya kumsafirisha hospitalini hali ilipozidi. Mchezaji huyo alikuwa katika hali mahututi alipoachwa hospitalini huku akitajwa kufariki Alhamisi asubuhi.

Taarifa kutoka kwa Royal Antwerp ilisoma ” Kutokana na heshima ya Joel na familia yake, klabu hii inaomba kupunguza mawasiliano. Muda wa maombolezi umeanza rasmi na klabu hii inaomba kuwasilisha rambirambi zake kwa familia ya Joel pamoja na marafiki.”

Wachezaji wenza waliokuwa mazoezini na Joel wamefanyiwa matibabu ya kiakili baada ya kushuhudia janga hilo la kuvunja moyo.

Klabu kadha kutoka Ubelgiji zimetwaa rambirambi zao zikiongozwa na Anderlecht iliyoandika ujumbe wa maombolezi kwenye Twitter kwa lugha ya Kifaransa na Kiingereza.

Lobanzo katika mechi ya awali

Royal Antwerp wamekuwa na uhusiano kwa muda mrefu na Manchester United hasa katika enzi za Sir Alex Ferguson. Kocha huyo alipendelea kuwatuma chipukizi wake huko Ubelgiji hasa wale aliojua watang’aa siku za usoni.

John O’Shea na Johnny Evans ni baadhi ya nyota wa Manchester United walioichezea Royal Antwerp kwa mkopo. Mwingine ni Dang Fangzhou .

 

John O’Shea

Leave a Comment