Mshambulizi wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Tottenham Harry Kane, amevunja rekodi ya mabao thelathini na sita iliyowekwa na Alan Shearer miaka ishirini na mbili iliyopita. Shearer alifunga mabao hayo akiwa na klabu ya Blackburn Rovers mwaka wa 1995.

Kane alifunga mabao matatu siku ya Jumanne Tottenham ilipoicharaza Southampton mabao matano kwa mawili, na kufikisha idadi ya mabao thelathini na tisa kwa ligi kuu ya Uingereza.

 

Nyota huyo alifunga bao la kwanza kwenye mechi hiyo dakika ya ishirini na mbili baada ya kukamilisha mkwaju wa adhabu uliochongwa na Cristian Eriksen.

Kane mwenye umri wa miaka 24, alisawazisha rekodi ya Shearer Jumamosi alipofunga mabao matatu dhidi ya Burnley kabla ya kumpita usiku wa Jumanne. Kane aliongeza bao la pili dakika ya thelathini na tisa kabla ya kucheka na wavu dakika ya sitini na saba tena.

Baada ya mabao hayo matatu dhidi ya Southampton, Kane ndio mfungaji bora mwaka huu kwa klabu na taifa lake kwani ana jumla ya mabao hamsini na sita huku Messi akiwa na hamsini na nne.

Kane ambaye ameshinda tuzo la mfungaji bora kwa misimu miwili kule Uingereza amesema kuwa ni fahari kubwa kulinganishwa na Messi au Ronaldo.

 

Muingereza huyo amepiga mabao matatu ( hat-tricks) kwa mara nane katika mashindano yote na mara sita kwenye Ligi kuu Uingereza mwaka wa 2017.

Kocha wake Mauricio Pochettino amesema kuwa Kane ndio mshambulizi bora kwani rekodi yake ni wazi. Hata hivyo, kocha huyo amemsihi aendelee kutia bidii ili awe bora zaidi. Nyota huyo alikiri furaha yake baada ya kuvunja rekodi hiyo anayosema ilikuwa ndoto yake.

Rekodi ya Alan Shearer imechukua miaka 22 kuvunjwa na hakuna anayejua itachukua muda upi kuvunja rekodi mpya iliyowekwa na Harry Kane. Hata hivyo inasikitisha kuwa wafungaji bora kama Alan Shearer huambulia patupu hasa kwenye tuzo za Ballon D’Or.

 

Wafungaji wengine waliotia fora ni Ruud Van Nistelrooy aliyekuwa Manchester United, Les Ferdinand kati ya wengine.
Tunasubiri kuona tuzo atakalopata Harry Kane kwani washambulizi kama Robin Van Persie, Thierry Henry walijaribu kuivunja ila wakalemewa.

 

Kane sasa anaongoza orodha ya wafungaji bora inayojumuisha Robert Lewandoski wa Bayern Munich, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Lionel Messi wa Barcelona na Edinson Cavani wa Paris Saint Germain.

Huu hapa ni ujumbe wa hongera kwa Harry Kane kutoka kwa Alan Shearer baada ya rekodi yake kuvunjwa.

 

 

Alan Shearer

@alanshearer
You’ve had a magnificent 2017 @HKane. You deserve to hold the record of most @premierleague goals in a calendar year. Well done and keep up the good work. 👏🏻🙋🏼‍♂️
3:55 PM – Dec 26, 2017
820 820 Replies 12,320 12,320 Retweets 54,374 54,374 likes
Twitter Ads info and privacy
.https://twitter.com/alanshearer

Leave a Comment